The Zuri Initiative
Sehemu 01 Kuwalinda Watoto Wakati Wa Covid 19
The Zuri Initiative yawaletea msururu wa video zenye mawaidha ya kujikinga, nyakati hizi za korona. Kwanza kabisa ni video hii inayoelezea jinsi ya kuwalinda watoto kutokana na maambukizi ya korona.
Leo, ningependa tuongee juu ya vile tunaweza kuwalinda watoto, wakati huu wa corona.
Wakati huu ambapo shule zimefungwa na watoto wako nyumbani, kama mzazi, pengine unajiuliza, ni jinsi gani utaweza kumlinda mtoto wako kutokana na hii corona virus. Katika video hii, nitakupa tips kadhaa za kukusaidia kuwalinda watoto wako kutokana na maambukizi ya corona.
Tip ya kwanza: Osha mikono yao mara kwa mara
Hakikisha watoto wanaosha mikono yao kwa kutumia maji na sabuni angalau kwa sekunde ishirini. Hiii ni muhimu sana, kwanza kama wametoka mahali public. Kuwasaidia watoto wachangamkie uoshaji wa mikono, mnaweza kutafuta wimbo wa kuimba kila mnapo osha mikono.
Tip ya pili: Waasaidie kuweka social distance
Jaribu kupunguza muda ambao watoto wanatumia kucheza kule njia. Pia, iwapo watu karibu nawe wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa COVID-19, ni vyema uchukue tahadhari ya kuwatenganisha watoto wako na watu hao .
Tip ya tatu: Wanunulie maski
CDC, ambayo ni Center for Disease Control inashauri kuwa watoto walio na miaka miwili na zaidi wanapaswa kuvaa maski, inayofunika mdomo na pua, kila wanapokua katika public places.
Tip ya nne: Sisitiza hatua za kujikinga
Waeleze watoto umuhimu wa hatua kama uoshaji wa mikono, kuweka social distance na kuvaa maski. Waeleze kuwa hatua hizi zitasaidia kuzuia wasiambukizwe corona. Pia, kama mzazi, kuwa mfano mwema kwa watoto wako. Wakikuona ukichukua hatua hizi kujilinda kutokana na maambukizi ya corona, itakua rahisi kwao kuiga mfano wako.
Tip ya tano : Hakikisha watoto wanafanya mazoezi ya kimwili
Mazoezi ya kimwili yanachangia sana afya njema kwa watoto . Hivyo basi, hakikisha kuwa watoto wanapata nafasi ya kufanya mazoezi ya kimwili.
Tamati
Ni hayo tu kwa leo. Iwapo una mawaidha mengine ya kutusaidia kulinda watoto wakati huu wa corona, tafadhali tujulishe, kupitia kwenya mitandao yetu ya kijamii. Kufikia hapo, sina la ziada. Zidi kukaa salama na kurembeka, kwa kutumia bidhaa za nywele za Zuri.
Kumbukumbu:
https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-nco